Klabu ya soka ya Sunderland imefanikiwa kupata
ushindi wa kwanza wakiwa ugenini baada ya kuifunga Crystal Palace 1-0 katika
mchezo mmoja wa Ligi Kuu England uliopigwa usiku wa jana.
Bao pekee la ushindi la Sunderland lilifungwa na
Jermain Defoe.
Ushindi huo umewaweka Sunderland katika nafasi ya 18
wakiwa na Pointi 9 baada ya kucheza mechi 13.
Ligi ya England inatarajia kuendelea tena Jumamosi
ya Novemba 28 kwa michezo mbalimbali ambapo, Aston Villa watakuwa wenyeji wa
Watford.
Bournemouth watawaalika Everton, Crystal Palace
watawakaribisha Newcastle, Man City watakuwa wenyeji wa Southampton, Sunderland
wataumana na Stoke huku Leicester city wakiwakaribisha Man United.
0 comments:
Post a Comment