TAIFA STARS YAANZA MCHAKAMCHAKA AFRIKA KUSINI
JOHANNESBURG, Afrika Kusini
Timu ya soka ya taifa ya Tanzania,Taifa Stars imeanza mazoezi yake nchini Afrika Kusini ikijianda na mchezo dhidi ya Algeria wa kuwania nafasi ya kuingia kwenye makundi ya kusaka tiketi ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwaka 2018 nchini Uswis.
Timu hiyo ilisafiri jana asubuhi kuelekea nchini humo kwa lengo la kuweka kambi ya siku 10 ambayo itafikia tamati Novemba 11 mwaka huu na kisha kurejea nchini kwa ajili ya mechi dhidi ya Mbweha hao wa Jangwa itakayochezwa Novemba 14 mwaka huu kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Akizungumza na mpanduka.blogspot.com kwa njia ya simu kutoka katika kambi ya mazoezi ya timu hiyo nchini Afrika Kusini, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la soka nchini TFF, Ahmed Msafiri Mgoyi alisema tangu timu iwasili nchini humo jana Jumatatu, ilifanya mazoezi mara moja(alasiri) na leo imefanya mazoezi mara mbili asubuhi na jioni.
"Hali ya hewa ya huku ni ya wastani, si baridi sana na wala si joto sana kama Dar es salaam, na hii inaiwezesha timu kufanya maandalizi yake vizuri zaidi.asuhuhi kuna baridi, mchana jua linawaka kidogo na jioni baridi hurejea tena," alisema Mgoyi.
Kikosi cha Taifa Stars kilichopo nchini humo kinawakilishwa na makipa Ally Mustafa (Yanga), Aishi Manula (Azam) na ,Said Mohamed (Mtibwa Sugar).
Mabeki wa pembeni ni Kessy Ramadhan na Mohammed Hussein (Simba), Juma Abdul na Haji Mwinyi (Yanga) na Shomari Kapombe (Azam).
Mebeki wa kati Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Hassan Isihaka (Simba), Kelvin Yondani na Nadir Haroub (Yanga).
Viungo Salum Telela (Yanga), Salum Abubakar, Himid Mao, Mudathir Yahya na Frank Domayo (Azam), Jonas Mkudena Said Ndemla (Simba).
Washambuliaji Farid Musa (Azam), Saimon Msuva (Yanga) na Mrisho Ngasa (Free State Stars-Afrika Kusini), John Bocco (Azam) na Elius Maguri (Stand United).
0 comments:
Post a Comment