Mwenyekiti wa Baraza la michezo kwa ukanda wa Afrika Mashariki na kati Leodegar Tenga atatetea nafasi yake ya uenyekiti wa Baraza hilo katika uchaguzi mkuu utakaofanyika siku ya ijumaa ya Novemba 20 mwaka huu katika mji wa Addis Ababa nchini Ethiopia.
Tenga amekuwa madarakani tangu mwaka 2007
alipochukua nafasi ya mwenyekiti wa CECAFA wa wakati huo Dennis Obua toka
nchini Uganda.
Tenga atakumbana na upinzani mkali kutoka kwa
wagombea wengine wanaowani Uenyekiti wa CECAFA ambao ni bosi wa zamani wa Shirikisho
la soka nchini Uganda (FUFA) Lawrence Mulindwa.
Wagombea wengine ni pamoja na Vincent Nzamwita
(Rwanda), Mutasim Sirelkhatim Gaffar wa (Sudan) na Juneid Bashar Tilmo wa
Ethiopia.
0 comments:
Post a Comment