ARSENAL YAMUWANIA CHICHARITO

Klabu ya Arsenal inaripotiwa kuwa inapanga kufanya usajili wa kushtusha wa Javier Hernandez ambaye amekuwa katika kiwango bora toka aondoke Manchester United na kutua Bayer Leverkusen ya Ujerumani.

Nyota huyo wa kimataifa wa Mexico aliondoka Old Trafford kwa kitita cha paundi milioni saba baada ya kuambiwa na meneja Louis van Gaal kuwa hayuko katika mipango yake msimu huu. Toka atue Bayer, Chicharito ameshafunga mabao 19 katika mechi 21 hivyo kumshawishi Wenger kumuwania ili aweze kusaidiana na Olivier Giroud.

Inaaminika kuwa nyota huyo anapenda kurejea Ligi Kuu na kama uhamisho ukifanikiwa ataungana na Danny Welbeck ambaye walikuwa wote United
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment