Na Arone Mpanduka
Waingereza huamini kwamba timu inayoongoza Ligi hadi
katika sikukuu ya Krismasi ndiyo itakayokuwa bingwa mwisho wa msimu.
Hapo jana, Disemba 25 ulimwengu umeshuhudia timu changa
ya Leicester City ikiwa kileleni mwa msimamo wa Ligi kuu ya Uingereza kwa kuwa
na pointi 38.
Imani hiyo imejitokeza katika ligi mbalimbali za
mpira wa miguu nchini humo ikiwemo Ligi Kuu ya Uingereza ambapo hadi kufikia
Krismasi huangaliwa timu inayoongoza katika msimamo na kisha hutabiriwa kuwa
bingwa.
Mara kadhaa mambo hayo yamekuwa yakijitokeza na kuwa
kweli, na ndiyo maana inapokaribia sikukuu ya Krismasi kila timu hupambana
kuhakikisha inasherehekea siku hiyo ikiwa ipo kileleni mwa msimamo.
Waingereza huamini kwamba kuongoza Ligi katika siku
hiyo ni baraka tosha ya ubingwa wa Ligi.
Katika misimu sita iliyopita ni timu moja tu ambayo
iliongoza Ligi wakati wa sikukuu ya Krismasi lakini mwishoni mwa msimu ikakosa
taji.
Timu hiyo ni Liverpool katika msimu wa 2013/2014
ambapo mwisho ilimaliza ligi ikiwa katika nafasi ya pili.
Hebu tuombe uzima na kuvuta subira ili tuone
kitakachotokea mwishoni mwa msimu huu kulingana na imani za hawa Waingereza.
0 comments:
Post a Comment