NDOA YA YANGA NA NIYONZIMA YAVUNJIKA RASMI

Hatimaye uongozi wa Yanga, umetangaza kuvunja rasmi mkataba wa kiungo wake Haruna Niyonzima.

Yanga imechukua uamuzi huo ikiwa ni miezi isiyozidi mitano tangu asaini mkataba mpya wa miaka miwili na Niyonzima.

Msemaji wa Yanga, Jerry Muro amesema Niyonzima atalazimika kulipa kiasi cha dola 71,175 (zaidi ya Sh milioni 149) kutokana na kukiuka mkataba uliosababisha kuvunjika kwa mkataba huo.

Mzozo wa Yanga na Niyonzima ulianza baada ya kiungo huyo kuchelewa kurejea kazini alipokwenda kuitumikia timu yake katika michuano ya Chalenji nchini Ethiopia.

Uongozi wa Yanga ulimsimamisha kwa madai amekuwa na tabia hiyo ya kuchelewa kila mara.

Tayari kiraka cha Niyonzima kilionekana kuzibwa na Thabani Kamusoko ambaye ameonyesha uwezo mkubwa katika msimu huu.

Mbali na kuimudu vema nafasi ya kiungo.Kamusoko pia ana uwezo wa kufunga mabao.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment