Wakala wa mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano
Ronaldo amedai kuwa nyota huyo bado ataendelea kuitumikia timu hiyo mpaka
atakapofikisha miaka 40.
Ronaldo mwenye umri wa miaka 30 na mshindi wa tuzo
tatu za Ballon d’Or amekuwa akihusishwa na tetesi za kwenda Paris Saint-Germain
au klabu yake ya zamani ya Manchester United kabla hajatundika daruga zake.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno ana mkataba na
Madrid unaomalizika Juni mwaka 2018, lakini Mendes amesisitiza mteja wake bado
anaweza kuendelea kubakia Santiago Bernabeu kwa muongo mwingine mmoja.
Jorge Mendes akipokea tuzo ya wakala bora wa mwaka
katika sherehe za Globe Soccer zilizofanyika huko Dubai jana.
Mendes amesema Ronaldo ndio mchezaji bora wa wakati
wote na ana uhakika kuwa anaweza kucheza kwa miaka mingine zaidi ya saba akiwa
Madrid.
Wakala huyo aliendelea kudai kuwa ana furaha
kuitumikia klabu hiyo na atastaafu akiwa na umri wa miaka 40.
0 comments:
Post a Comment