AZAM FC YATOLEWA MAPINDUZI CUP

Azam FC imeungana na Mafunzo kuiaga michuano ya Mapinduzi baada ya jioni ya leo kuchapwa mabao 2-1 kwenye uwanja wa Amaan.

Azam ndiyo walioichokoza Mafunzo kwa bao la dakika ya 20 lililofungwa na Kipre Tchetche.

Lakini baadae Mafunzo ikasawazisha na kufunga la pili kupitia kwa Makame.

Kufuatia kipigo hicho Azam imeambulia pointi mbili ilizopata katika sare mbili huku Mafunzo pia ikiwa imeambulia pointi tatu na kupoteza mechi mbili za awali.

Kwa mtaji huo zote zimeungana kuipa kisogo michuano hiyo
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment