KAIJAGE AJIUZULU TWIGA STARS

Kocha mkuu wa timu ya soka ya taifa ya wanawake Twiga Stars Rogasian Kaijage ametangaza kumwaga manyanga ya kuifundisha timu hiyo.

Kocha huyo ameandika kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa facebook leo hii akielezea kuachana na timu hiyo kama ushahidi unavyoonekana hapo chini.

Kwa kipindi kirefu Kaijage alikuwa akililalamikia Shirikisho la soka nchini TFF kwa kuitelekeza timu hiyo kufuatia kutoipa matunzo ikilinganishwa na timu ya taifa ya wanaume, Taifa Stars.

MPANDUKA BLOG ilimpigia simu kocha huyo lakini alionyesha kutokuwa tayari kutolea ufafanuzi taarifa hiyo ya facebook.

"Mpigie Kizuguto(Afisa Habari wa TFF), yeye ndiyo anaweza kuwa na taarifa kamili kuhusu mimi ila binafsi siwezi kukueleza chochote,"alisema.

Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment