SIMBA SC CHUPUCHUPU KUZAMA ZENJI

Simba imeanza michuano ya Mapinduzi kwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Jamhuri ya Pemba katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar usiku huu.

Awadhi Juma ndiye alikuwa wa kwanza kufunga bao katika dakika ya 12.

Hata hivyo Jamhuri wakasawazisha dakika ya 18 kupitia kwa Mwalimu Mohammed aliyefunga akitumia udhaifu wa mabeki Jonas Mkude na Mohammed Fakhi.

Jamhuri ilipata bao la pili kupitia kwa Ammy Bangekesa  katika dakika ya 52 ya mchezo.

Katika dakika za mwisho Awadhi Juma akafunga bao la kusawazisha kwa Simba na kufanya sare ya 2-2.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment