YANGA YALINDA HESHIMA KWA MTIBWA

Yanga imefanikiwa kuifunga Mtibwa Sugar usiku huu mabao 2-1 katika mchezo kombe la Mapinduzi uliochezwa kwenye uwanja wa Amaan Zanzibar.

Ushindi huo kwa Yanga ni wa kujiwekea heshima kwani tayari imefuzu hatua ya robo fainali baada ya Azam na Mafunzo kutolewa mapema kwenye kundi lake.

Mtibwa nayo licha ya kufungwa haina cha kupoteza kwa sababu nayo pia imefuzu robo fainali.

Mabao ya Yanga yamefungwa na Boubacar Garba dakika ya 42 na Malimi Busungu dakika ya 81.

Garba alifunga bao la kusawazisha baada ya Mtibwa kutangulia kufunga katika dakika ya 10 kupitia kwa Kichuya.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment