Shirikisho la soka nchini TFF leo(Alhamis Feb
4,2016) imefanya maajabu mengine baada ya kubadili ratiba ya Ligi Kuu ya mechi
ya JKT Ruvu na Mbeya City kwa kuianzisha mapema ili kupisha mechi ya kirafiki
kwenye dimba la Karume jijini Dar es salaam.
Kwa kawaida ratiba ya mchezo huo ilikuwa inaonesha
kwamba JKT Ruvu na Mbeya City ni saa 10 jioni lakini TFF ikaurudisha nyuma
mchezo huo na kuufanya uanze saa 9 alasiri kwa lengo la kupisha mchezo wa
kirafiki usiotambulika na TFF kati ya Clouds Media na Majaji.
Mabadiliko hayo yamezua malalamiko mengi katika
mitandao ya kijamii huku wengine wakidai kwamba viongozi wa Shirikisho hilo
wameshindwa kuongoza soka la Tanzania.
Ikumbukwe kuwa mwezi uliopita TFF ilifanya kosa kwa
kuiruhusu Azam FC kuacha mechi zake za Ligi kuu na kwenda nchini Zambia kucheza
mechi za kirafiki, jambo ambalo Rais Jamal Malinzi aliomba radhi.
Katika mchezo huo wa leo kati ya JKT Ruvu na Mbeya
City, Mbeya imeshinda mabao 2-1.
0 comments:
Post a Comment