UWANJA WA TAIFA UMEJAA, MASHABIKI WAOMBWA KUBAKI NYUMBANI

Uwanja wa taifa tayari umejaa na watu hawaruhusiwi tena kuingia.

Kwa mujibu wa Afisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la soka nchini Alfred Lucas, mageti ya uwanja huo yamefungwa baada ya uwanja kujaa tangu saa tano na nusu asubuhi.

Lucas amewaomba mashabiki walioko nyumbani wasihangaike tena kwenda uwanjani.

Mchezo kati ya Yanga na TP Mazembe utaanza saa 10 kamili jioni ambapo Azam TV na Supersport 9 wataonyesha.

Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment