WANASIMBA WA ZENJI WASIKITISHWA NA KICHAPO CHA YANGA

Licha ya watani zao wa jadi Yanga kupoteza mchezo wa pili wa hatua ya nane bora ya Kombe la Shirikisho, wapenzi wa Simba visiwani Zanzibar waelezea kusikitishwa na matokeo hayo.

Jumanne Yanga ilikubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa TP Mazembe ya Congo DR kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Akizungumza na MPANDUKA BLOG kiongozi wa klabu ya Simba kwa upande wa Zanzibar Abdul Mshangama alisema Yanga inaiwakilisha Tanzania hivyo kufungwa kwao ni kama Tanzania imefungwa.

"Yanga imetusikitisha licha ya kwamba wakati mwingine inatudharau na kutuita majina ya ajabu kama wa mchangani," alisema Mshangama.

Alisema anaitakia kila lakheri kuelekea kwenye mchezo wake mwingine dhidi ya Medeama ya Ghana.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment