JOSEPH OMOG ASAINI MIAKA MIWILI MSIMBAZI

Kocha Mkameruni Joseph Omog amesaini mkataba wa miaka miwili kuionoa Simba ya Dar es Salaam.

Mkataba huo utaisha mwaka 2018.

Omog amesaini mkataba huo leo kwenye hoteli ya Regency jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari akiwa pamoja na Rais wa Simba, Evans Elieza Aveva.

Omog amesema anaujua ukubwa wa Simba na changamoto zake na amesisitiza atapambana kuhakikisha anaipa mafanikio timu hiyo.

Omog amesaini mkataba huo baada ya kutua nchini usiku wa jana.

Katika mkutano huo na waandishi wa habari, Rais Aveva pia ameutumia kumtambulisha rasmi Patrick Kahemele kuwa Katibu mpya wa klabu ya Simba.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment