URENO YATINGA NUSU FAINALI EURO 2016

Ureno imefuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya Euro kwa changamoto ya mikwaju ya penati 5-3 dhidi ya Poland baada ya sare ya 1-1 ndani ya dakika 120.

Ricardo Quaresma alikwamisha penati ya mwisho ya kuipa ushindi Ureno baada ya mkaju wa Jakub Blaszczykowski kuokolewa.

Robert Lewandowski alianza kuifungia Poland bao la kuongoza kwa kichwa dakika ya pili tu tangu mchezo huo uanze lakini kinda wa Ureno Renato Sanches alisawazisha badae kabla ya mapumziko.

Ureno inatarajia kukutana na Wales au Ubelgiji kwenye hatua ya nusu fainali, timu hizo zitakuna Ijumaa kwenye mchezo robo fainali.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment