Klabu ya soka ya Chelsea imetangaza rasmi kwamba
imenasa saini ya kiungo wa Leicester City, N’golo Kante kwa ada ya pauni
milioni 30.
Kante mwenye umri wa miaka 25 amesaini mkataba wa
miaka mitano na atakuwa akipokea mshahara wa pauni 120,000 kwa wiki akiwa
darajani.
Kante alifanya vizuri sana msimu uliopita akiwa na
Leicester City na kuwa mmoja wa wachezaji waliochangia timu hiyo kutwaa taji la
Ligi Kuu England.
0 comments:
Post a Comment