Mchezaji tenisi namba moja Duniani kutoka Serbia,
Novak Djokovic amemaliza msimu wake kwa ushindi dhidi ya Roger Federer.
Ushindi huo umemfanya kuweka rekodi ya taji la nne
mfululizo la mashindano ya ATP.
Djokovic alifanikiwa kushinda kwa seti 6-3, 6-4 katika
dakika 80 za mchezo huko London, na aliweza kusahihisha makosa yake baada ya
mechi ya mwanzo ya makundi kufungwa na Roger Federer.
Mpaka sasa Djokovic anamaliza mwaka huu kwa kushinda
mataji 11 yakiwemo ya matatu ya Gland slam, na kwa upande wake Roger Federer
amesema hakuna furaha yoyote katika upande ulioshindwa ila ni vizuri kushiriki
kuliko kutoshiriki kama mwaka uliopita.
0 comments:
Post a Comment