Timu ya taifa ya waendesha baiskeli kutoka Rwanda
imenawiri katika mashindano ya kimataifa ya Tour of Rwanda yaliyomalizika mjini
Kigali.
Timu ya Rwanda imetetea ubingwa wa mashindano hayo ya
Tour of Rwanda.
Jean Bosco Nsengimana mwenye umri wa miaka 22
ameibuka mshindi wa mashindano hayo yaliyofanyika Rwanda kwa wiki nzima
yakishirikisha jumla ya waendesha baiskeli 60 kutoka kona zote duniani.
Nsengimana aliwashinda nguvu wenzake wa timu ya
Rwanda Joseph Aleluya aliyemaliza katika nafasi ya pili na Camera Hakuzimana
aliyechukua nafasi ya tatu.
Hii ni mara ya pili mfululizo waendesha baiskeli hao
kutoka Rwanda kunyakua taji kuu katika mashindano hayo ya Tour of Rwanda
yaliyoko kwenye kalenda ya mashindano ya mbio za baiskeli barani Afrika
yanayotambuliwa na shirikisho la dunia la mbio za baiskeli.
0 comments:
Post a Comment