YANGA POAA, SIMBA 'VEPEE?'

Ligi kuu soka Tanzania Bara imeendelea tena leo kwa michezo kadhaa ambapo kwenye dimba la Taifa jijini Dar es salaam Yanga imeweza kuishindilia Mbeya City mabao 3-0.

Mabao ya Yanga yamefungwa na Amis Tambwe dakika za 36 na 65 huku Kamusoko akifunga la tatu dakika ya 66.

Kule Shinyanga Simba ilikuwa imealikwa na Mwadui FC ambapo mchezo umekwisha kwa sare ya 1-1.

Mwadui walianza kufunga kupitia kwa mchezaji wa zamani wa Yanga Nizar Khalfan kabla ya Brian Majwega kusawazisha.

MATOKEO MENGINE
Mtibwa Sugar 3-0 Mgambo JKT.

Ndanda FC 1-1 JKT Ruvu

Coastal Union 1-3 Stand United

Majimaji 0-2 Prisons
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment