Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa
Stars na klabu ya TP Mazembe ya Congo DR, Mbwana Samatta usiku wa leo atachuana
na wachezaji wenzake katika kinyang’anyiro cha tuzo ya mchezaji bora wa Afrika
anayecheza ndani ya bara hilo.
Tuzo hizo zitafanyika mjini Abuja nchini Nigeria
ambapo Samatta amesindikizwa na wadau kadhaa wa soka kutoka Tanzania akiwemo
Katibu mkuu wa Shirikisho la soka nchini TFF, Mwesigwa Celestine.
Muda wa kuanza sherehe hizo ni saa 4:30 usiku kwa
saa za Afrika Mashariki.
Samatta alionyesha umahiri mkubwa katika soka hasa
upachikaji mabao katika kipindi chote cha mwaka 2015 ikiwemo kuiongoza klabu
yake ya TP Mazembe kutwaa ubingwa wa vilabu barani Afrika.
Mbali na hilo Samatta aliibuka kuwa mfungaji bora
katika fainali hizo kwa kufikisha jumla ya mabao saba.
Wanowania tuzo ya mchezaji bora wa
mwaka kwa wachezaji wanaocheza nje ya
bara la Afrika ni Andre Dede Ayew wa
Ghana/Swansea City, Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon/Borussia Dortmund na
Yaya Toure wa Cote
d"Ivoire/Manchester City.
TUZO ZINGINE
Mchezaji Bora Kijana wa Mwaka
Kipaji kipya
Kocha wa Mwaka
Mwamuzi bora wa Mwaka
Timu ya Taifa Bora ya Mwaka
Timu ya Taifa Bora ya Mwaka ya wanawake
Klabu ya Mwaka
0 comments:
Post a Comment