CHILE MABINGWA COPA AMERICA, ARGENTINA FUNGU LA KUKOSA

Chile imeichapa Argentina kwa mikwaju ya penati 4-2 kwenye fainali ya michuano ya Copa America Centenario na kulitetea taji lao walilolitwaa mwaka 2015, baada ya kushuhudia dakika 120 zilizomalizika bila miamba hiyo ya soka la Amerika ya Kusini kufungana.

Baada ya Sergio Romero kupangua mkwaju wa penati ya kwanza ya Chile iliyopigwa na Arturo Vidal, Lionel Messi aliishuhudia penati yake ikigonga ‘mtambaa panya’ na kuirudisha Chile mchezoni.

Golikipa wa Chile Claudio Bravo naye akaokoa mchomo wa penati ya Lucas Biglia wa Argentina kabla ya Francisco Silva kukandamiza mkwaju wake kambani na kuitangaza Chile bingwa wa michuano hiyo.

Gonzalo Higuain Higuani alikaribia kupa bao timu yake mapema dakika ya 21 baada ya Chile kufanya makosa kwenye safu yao ya ulinzi. Striker huyo wa Napoli akiwa yeye na golikipa, mpira aliou-chop ulitoka nje kidogo ya goli.

Dakika chache baadaye, Nicolas Otamendi alipata nafasi nyingine ya kuzifungua nyavu za Chile, lakini mpira alioupiga kwa kichwa kuunganisha free-kick ya Messi ulipiga nyavu za pembeni.

Dakika ya 28, Marcelo Diaz wa Chile alioneshwa kadi ya pili ya njano kisha kutolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea vibaya Messi na kuwaacha Chile wakipambana na Argentina huku wao wakiwa 10 uwanjani.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment