KOCHA MWINGINE WA NIGERIA AFARIKI DUNIA

Siku tatu baada ya kifo cha aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Nigeria Stephen Keshi, Mkurugenzi wa Ufundi wa timu ya taifa ya vijana ya nchi hiyo Amodu Shaibu amefariki dunia.

Shaibu ambaye pia aliwahi kuifundisha timu ya taifa ya Nigeria kwa nyakati tofauti, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo akiwa usingizini.

Inaelezwa kuwa marehemu alikuwa akilalamika kusumbuliwa na maumivu ya kifua jana jioni.

Mwili wake umehifadhiwa kwenye hospitali ya Stella Obasanjo ambayo pia mwili wa Keshi umehifadhiwa huko.

Enzi za uhai wao, Shaibu na Keshi walikuwa wakipokezana kijiti cha kuinoa Super Eagles mara kwa mara.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment